News Archive

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limetoa semina  juu ya umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa wanachama wa kikundi cha Umoja wa Miradi ya Viziwi Tanzania, UMIVITA. Semina hiyo ilifanyika siku ya Jumapili ya tarehe 07/05/2017 katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la NSSF Mafao House, Ilala jijini Dar es Salaam na ilihusisha wanachama wapatao mia mbili.

 

Akizungumza katika semina hiyo Ofisa Matekelezo Mkuu wa NSSF Mkoa wa Temeke, Nuhu Ramadhani alisema wanachama hao walipata fursa ya kuifahamu vizuri NSSF na kujua mafao yanayotolewa na shirika hilo yakiwemo pensheni ya uzeeni,pensheni ya ulemavu,pensheni ya urithi, msaada wa mazishi, mafao ya kuumia kazini, mafao ya uzazi na matibabu bure kwa mwananchama na wategemezi wake.

Wanasemina wakipewa  vipeperushi vyenye taarifa kuhusu Mafao yatolewayo na NSSF

Baadhi ya wanasemina wakifatilia kwa makini mada ya umuhimu wa Hifadhi ya Jamii.

 

Aidha NSSF ilitoa fursa kwa Wanachama wa UMIVITA waliohudhuria semia hiyo kujiandikisha kuwa wanachama.

Ofisa wa NSSF akiwaandikisha baadhi ya wanachama wa UMIVITA kujiunga na NSSF.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4