News Archive

Shirika la Taifa La Hifadhi ya Jamii, NSSF limeshiriki katika maonesho ya Kimataifa ya biashara yaliyofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Sabasaba yalioanza tarehe 28/06/2017 na kumalizika tarehe 13/07/2017.

 

Katika Maonesho hayo, NSSF ilitoa huduma mbalimbali muhimu kwa wanachama wake na wananchi wote waliopita kwenye banda hilo. Huduma zilizotolewa katika banda la NSSF ni pamoja na kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa umma, kuandikisha wanachama wapya na kutoa kadi papo hapo. Wanachama pia waliweza kupata taarifa za michango yao. NSSF pia ilipokea maoni na malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali na kuwatafutiau ufumbuzi wa haraka.

Kadhalika NSSF ilitoa huduma za kupima afya bure (kwa magonjwa yasiyoambukiza) pamoja na kutoa ushauri wa kiafya kwa walio pima afya zao. Sambamba na kupima afya, kulikuwa na huduma za uchangiaji damu.

Kaulimbiu ya maonesho ya mwaka huu ilikuwa‘’UKUZAJI WA BIASHARA KWA MAENDELEO YA VIWANDA’’ ambapo NSSF tayari ni mdau mkubwa sana katika kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwenye swala la kukuza viwanda. Kwa kuzingatia hayo ndani ya banda la NSSF kulikuwa na wawakilishi wa viwanda mbalimbali ambavyo Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii imewawezesha kufufua, kuanzisha na kukuza viwanda vyao.Wadau wa viwanda waliokuwa ndani ya banda la NSSF ni pamoja na Kiwanda cha Viuwadudu Kibaha, Bodi ya nafaka mchanganyiko CPB, Kiwanda cha Chaki cha Maswa pamoja na benki ya Azania.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4