News Archive

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Bwana William Erio (kulia) akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Wa Hifadhi Ya Jamii Na Bima wa Sierra Leone Bwana  Mohammed Gondowe aliyetembelea leo  katika Makao Makuu ya ofisi ya NSSF iliyopo jijini Dar es salaam.

Nchi ya Sierra Leone imefurahishwa na  na hatua kubwa  ya maendeleo yanayofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi  ya Jamii NSSF   nchini  na kwamba italazimika kuiga baadhi ya masuala  ikiwemo kuanzisha kitengo kipya  cha viatarishi   katika mfuko wao ili kuongeza ufanisi na kuzuia kutokea kwa  majanga yanayoweza kujitokeza .

Hayo yamesemwa  na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi  ya Jamii na Bima SIERRA LEONE  bwana Mohammed Gondoe alipotembeelea katika  makao makuu ya NSSF jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Taifa  la Hifadhi ya Jamii NSSF, Bwana William Erio ambapo amesema kuna mambo mazuri yamefanywa na NSSF hivyo hawana budi kujifunza .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NSSF William Erio amesema Tanzania na SIERRA LEONE zitaendelea kushirikiana na kuwa na mahusiano  mazuri katika kuhakikisha wanabuni mipango ya kusaidia ukuaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Taifa.

Mifuko ya Hifadhi ya jamii ya TANZANIA  na SIERA LEONE imekuwa ikishirikiana kwa muda mrefu   jambo ambalo limesaidia kuongeza ufanisi na weledi  katika utendaji kazi wake  kwa wafanyakazi wa mifuko hiyo.

Bwana Gondoe  na wajumbe wenzake kutoka nchini SIERRA LEONE wapo nchini  kujifunza  masuala mbali mbali  ya hapa nchini ikiwemo  mfumo  wa utoaji  mikopo ya elimu ya juu uliopo chini ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4