Uandikishaji wa Wanachama

Mwajiri yeyote anawajibika kuwaandikisha wafanyakazi wake wote alionao na kupewa namba za uanachama ambazo ni lazima kwa mwanachama kuitunza namba hiyo. Mwanachama anawajibika kupewa kitambulisho cha uanachama NSSF/R4 ambacho kinatumika kwa ajili ya kupata mafao na huduma yoyote nyingine kutoka katika Shirika.

Uandikishaji Wanachama wa Hiari

Mtu yeyote aliyejiajiri, mkulima, mfanyakazi wa ndani, wafanya biashara wadogo wadogo wanaweza kujiandikisha kwa hiari na kulipia kadiri ya uwezo wake kuanzia shilingi 20,000 kwa mwezi (asilimia 20 ya mshahara wa kima cha chini (KCC) wa serikali) na atapata mafao yote saba yatolewayo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii..

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1