emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

NSSF Schemes

Wavuvi Scheme


Malengo

 • Kuwakinga wavuvi dhidi ya majanga kwa kuwapa mafao yote Yatolewayo na NSSF
 • Kuwapa wavuvi na familia zao matibabu ya bure ili wawe na afya bora ya kuweza kuzalisha kwa ufanisi zaidi.
 • Kusaidiana na serikali kupunguza umaskini kwa jamii.kujenga Kizazi kisicho tegemezi kwa kutoa pensheni ya uzee, urithi na Ulemavu na kupambana na umasikini kwa ujumla.
 • Kuwawezesha wavuvi kupata mikopo ya riba nafuu sana kwa ajili ya kununulia pembejeo,kusomesha watoto wao, na shughuli nyingine za maendeleo.
 • Kunusuru kipato ambacho wangekitumia katika matibabu na badala yake wakitumie kujiendeleza kiuchumi
 • Kuwawezesha wavuvi kupata mafao ya pensheni wakati watakapokuwa wazee na kushindwa kuendelea na uvuvi.
 • Kuwaunganisha wavuvi kwa pamoja ili watambue kuwa wapo kwenye ajira yenye tija kwao, na hivyo wazidi kuithamini na kuiendeleza na hatimaye kuleta kipato kwao na kwa taifa kwa ujumla.
 • Kuwajengea wavuvi utamaduni wa kujiwekea akiba ili iweze kuwasaidia nyakati ambapo hakuna uzalishaji.

Wanaohusika Na Mpango Huu

 • Wanachama wote waliojiunga na vikundi shirikishi vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi (BMU) au vyama vingine vyovyote vya uvuvi
 • Mvuvi mmojammoja ilimradi awe na uhakika wa kuweza kuchangia japo Tshs. 20,000/- na zaidi kwa kila mwezi
 • Watu wote wanaojishughulisha na biashara zote za uvuvi ikiwemo ununuzi wa samaki, usafirishaji, usindikaji, uongezaji thamani (Fish prossessing), uuzaji wa samaki na yale yote yatokanayo na uvuvi wa samaki ambao hawapo katika ajira rasmi.
 • Watu wote wanaojishughulisha na uvuvi,ufugaji wa samaki ,pamoja na wale wote wanaojishughulisha na biashara zitokanazo na shughuli zilizotajwa hapo juu.

ULIPAJI MICHANGO:

 • Mwanachama wa sekta ya uvuvi atapaswa kulipa kiwango chochote ilimradi kisiwe chini ya (Tshs. 20,000/-kwa sasa.)
 • Michango hiyo itaanza tu mara mwanachama atakapoandikishwa.
 • Michango hiyo hulipwa kila mwezi bila kuruka. Mwanachama akiruka mwezi/miezi itambidi alipie miezi hiyo ili huduma/mafao hasa ya matibabu yaendelee.
 • Michango itapokelewa katika ofisi yoyote ya NSSF nchini na risiti itatolewa.
 • Michango hiyo pia inaweza kulipwa kupitia vyama vyao kwa namna ambayo watakubaliana wanachama,na NSSF sehemu husika.
 • Michango inaweza kuwasilishwa kwa mfumo wa simu M-PESA, TIGO PESA, NA AIRTEL MONEY kwa namba zitakazotolewa.
 • Mwanachama anaweza kulipa kwa miezi ya mbele,kwa msimu,au kwa mwaka mzima.