Saturday, May 25, 2013

Ulipaji wa Mchango

Mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii huchangiwa kati ya mwajiri na mfanyakazi kwa kiwango cha asilimia 20 (20%) ya mshahara wa mfanyakazi. Moja kati ya viwango vifuatavyo vinaweza kutumika kutegemeana na maamuzi ya mwajiri na mwanachama.

  1. 10% kwa mfanyakazi na 10% kwa mwajiri au
  2. 5% kwa mfanyakazi na asilimia 15% kwa mwajiri
Ulipaji wa Michango

Mwajiri ana wajibu wa kisheria wa kulipa michango ya wanachama wake ndani ya mwezi mmoja baada ya kulipa mishahara. Michango hulipwa kwa kujaza fomu maalumu ya michango na kuwasilishwa katika ofi si ya NSSF iliyo karibu nae. Mwajiri anaweza kulipa michango kwa njia ya fedha taslimu, cheki ya benki au uhamishaji wa kibenki (Bank transfer) kwa kutumia mfumo wa kompyuta.

Ufuatiliaji wa Mchango
Wajibu wa Kulipa Michango

Jukumu la kuhakikisha michango ya wanachama inalipwa kwa wakati ni lamwajiri mwenyewe na wafanyakazi wake. Hata hivyo ili kuhakikisha waajiri na wanachama wanajiandikisha na kulipa michango kwa wakati Shirika hutumia pia wakaguzi wake ambao hufanya ukaguzi kwa waajiri kila mara inapobidi

Aina za Ukaguzi

Kuna aina kuu tatu za ukaguzi ambao hufanywa na wakaguzi wa shirika katika kuhakikisha waajiri na wanachama wanatekeleza wajibu wao kisheria.

Ukaguzi wa Kawaida (Routine)

Huu ni ukaguzi unaofanyika mara mbili kwa mwaka kwa kila mwajiri.Katika ukaguzi huu mwajiri anawajibika kutoa taarifa zote zinazohusiana na wafanyakazi wake kwa ajili ya ukaguzi. Mkaguzi anayehusika atatoa taarifa rasmi ya kufanya ukaguzi huo kabla ya siku ya ukaguzi.

Ukaguzi Fuatilizi (follow up)

Huu ni ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa kwa lengo la kufuatilia jambo maalum kama michango isiyolipwa, adhabu iliyotozwa, hundi iliyorudishwa benki, uandikishaji wa wanachama, n.k.

Ukaguzi Chunguzi (Survey)

Huu ni ukaguzi unaofanywa kwa lengo la kugundua waajiri wasiojiandikisha katika Shirika ili kutimiza wajibu wao wa kisheria.

Adhabu

Iwapo mwajiri atachelewesha michango zaidi ya mwezi mmoja baada ya mwezi wa mishahara aslimia 5 ya mchango husika hutozwa kama adhabu kwa kila mwezi uliochelewa.