Thursday, June 20, 2013

Pensheni ya Uzeeni

nssf2

NSSF hutoa mafao ya pensheni ya uzeeni ambayo hulipwa kwa kila mwezi kwa mwanachama aliyetimiza sifa zifuatazo..

Sifa Zinazotakiwa:
  • Awe ametimiza umri wa kustaafu kwa hiari wa miaka 55 – 59 au kustaafu kwa lazima kwa miaka 60.
  • awe amechangia katika mpango wa hifadhi ya jamii si chini ya michango 180.
  • Kwa wanachama waliokuwa na umri mkubwa wakati NSSF inaanza wanao unafuu wa viwango vya michango inayotakiwa kama inavyooneshwa katika jedwali la hapa chini
nssf1
Mafao yanayotolewa

Pensheni ya uzee hupatikana kutokana na wastani wa mapato ya mwanachama kwa miaka mitano yenye michango mizuri/mikubwa katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho.

Kiwango cha Pensheni ya kuanzia ni 30% ya wastani wa mapato kwa mwanacahama aliyetimiza michango 180. Hata hivyo 1.5% huongeazwa kwa kila miezi 12 inyozidi 180 hadi kufikia kiwango cha juu kabisa cha 67.5% ya wastani wa mapato ya mwanachama.

Mafao yanayotolewa katika pensheni ya uzee ni;

  • Pensheni ya kila mwezi
  • Mkupuo wa awali kabla ya kuanza malipo ya pensheni ambao ni kiwango cha pensheni mara miezi 24
  • Mkupuo maalum kwa mwanachama aliyekosa sifa za pensheni yaani mchango wa mwisho mara idadi ya michango
  • Kiasi cha chini cha pensheni ni 80% ya Kima Cha Chini cha Mshahara (KCC) unaotangazwa na Serikali
  • Kiasi cha juu cha pensheni ni 67.5% ya wastani wa mapato ya mwezi.
Mfano wa Mahesabu ya Pensheni ya Uzee

 Tuchukue mfano wa mzee Mwendapole ambaye amestaafu akiwa na umri wa miaka 60 na mahesabu yake kupatikana kama ifuatavyo; [1/600*180+0.015(N - 15)]*AIME

N = Muda wa kuchangia (Miezi)

AIME = Wastani wa Mapato ya mwezi kwa kipindi cha miaka mitano ya mwisho

 Wastani wa mapato kwa mwezi ni Tshs 120,000

 Idadi ya michango wakati wa kustaafu ni 180

 Kiwango cha pensheni ya kuanzia ni 30%

 Hesabu ya pensheni yake itakuwa ni 120,000 x 30%= 36,000. Kwa kuwa hesabu ya pensheni yake iko chini ya 80% ya kima cha chini cha mshahara, hivyo pensheni ya Mzee Mwendapole itakuwa 80% ya KCC yaani Tshs 80,000 badala ya Tshs 36,000

 Mkupuo wa awali utakuwa Tshs 36,000 x 24 = 864,000 (b).

Tukichukua mfano wa kuwa wastani wa mapato ya Mzee Mwendapole ulikuwa Tshs 360,000 hivyo pensheni yake itakuwa Tshs 360,000 x 30% = 108,000 na mkupuo wake wa awali utakuwa Tshs 108,000 x 24 = 2,592,000 (c).

Tukichukua tena mfano kuwa mzee Mwendapole alistaafu akiwa na idadi ya michango 240, kiwango cha asilimia ya pensheni yake kitakuwa ni 37.5% yaani 30% + 1.5% x miaka 5 (miezi 60 iliyozidi 180).

Hivyo pensheni yake ya kila mwezi itakuwa Tshs 120,000 x 37.5% = Tshs 45,000 kwa mfano (a) hapo juu na ambayo bado iko chini ya 80% ya KCC na hivyo kulipwa pensheni ya Tshs 80,000 badala ya Tshs 45,000.

Kwa mfano wa (b) hapo juu pensheni yake itakuwa Tshs 360,000 x 37.5% = Tshs 135,000 Mkupuo wake wa awali pia utabadilika na kuwa Tsh 1,080,000 kwa mfano wa a) na Tsh 3,240,000 kwa mfano wa (b).