Wednesday, June 19, 2013

Pensheni ya Ulemavu

nssf3

Pensheni hii hulipwa kwa mwanachama aliyepoteza angalau 2/3 ya uwezo wake wa kufanya kazi kutokana na ulemavu wa kimwili au kiakili kama utakavyothibitishwa na Bodi ya Madaktari

Sifa Zinazotakiwa
  1. Uthibitisho wa Bodi ya Madaktari wa kupoteza 2/3 ya uwezo wa kufanya kazi.
  2. Michango 180 au angalau 36 kati yake michago 12 iwe imelipwa karibu na kupata ulemavu
  3. Awe chini ya umri wa kustaafu
Mafao yanayotolewa
  1. Ukokotoaji wa pensheni ya ulemavu ni sawa na ule wa pensheni ya uzee isipokuwa huongezwa 1% kwa kila michango 12 inayozidi kiwango cha michango 180
  2. Mafao yanayotolewa ni sawa pia na mafao ya pensheni ya uzee yaani pensheni ya kila mwezi, mkupuo wa awali na mkupuo maalum kwa aliyekosa sifa zinazotakiwa.
  3. Pensheni hulipwa hadi mwanachama atakapofariki au atakapotimiza umri wa kustaafu na kuhamia pensheni ya uzee.