
Mafao haya hulipwa kwa wanachama wanawake wanaotegemea kujifungua au wameshajifungua.
Mafao haya ni asilimia 100% ya wastani wa mapato ya siku ya mwanachama kwa kipindi cha miezi sita kabla ya wiki ya 20 ya ujauzito. Mafao haya hulipwa kwa muda wa wiki 12
Malipo hufanyika kwa awamu mbili yaani wiki 4 kabla ya kujifungua na wiki 8 baada ya kujifungua. Mwananchama anaweza kuamua kulipwa kwa wiki zote 12 baada ya kujifungua.
Matibabu hutolewa kwa magonjwa yanayoambatana na ujauzito wa mwanachama. Matibabu huanza kutolewa baada ya wiki ya 24 ya ujauzito na huishia masaa 48 baada ya kujifungua au siku 7 ikiwa nikujifungua kwa upasuaji. Matibabu haya hufanywa na hospitali ambazo zimeingia mkataba na Shirika wa kutibu wanachama wa NSSF