Tuesday, May 21, 2013

Uandikishaji wa Waajiri

Waajiri wanaohusika kisheria kuandikishwa katika mfumo wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF ni;

  • Waajiri wote walio katika sekta binafsi
  • Taasisi zisizokuwa za kiserikali
  • Ofi si za Kibalozi zinazoajiri Watanzania
  • Taasisi za Kimataifa zinazofanya shughuli ndani ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania
  • Taasisi na Wizara za Serikali zinazo ajiri wafanyakazi kwa masharti ya muda
  • Mashirika ya umma yanayoajiri wafanyakazi kwa masharti ya muda Watu binfsi waliojiajiri wenyewe
  • Sehemu yoyote ya shughuli kama itakavyotangazwa na Waziri anayehusika na kazi
Muda wa Kujiandikisha

Mwajiri yeyote anawajibika kujiandikisha katika shirika kama mwajiri mlipa michango na kupewa namba ya uandikishaji mara tu anapoanza shughuli zake.