
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau akikabidhiana mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigamboni na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CRJE Nd. Shi Yuan katika hafla fupi iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar Es salaam. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli , Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe Said Sadick na Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe Gaudentia Kabaka
Daraja hili litakuwa la urefu wa mita 680 na litajengwa upande wa Kurasini na kutua Vijibweni upande wa Kigamboni. Mradi huu umeshaanza tangu tarehe 1 February 2012 na matayarisho ya awali yanaendelea na ifikapo Mwezi Agosti mwaka huu daraja litaanza kujengwa rasmi
Daraja linategemewa kugharimu dola za kimarekani milioni 130/ Shilingi bilion 214 na litakuwa na barabara sita. Tatu za kwenda Kigamboni na tatu kurudi mjini....Daraja hili ni chachu ya miradi ijayo ya Shirika katika nyumba za bei nafuu kwa ajili ya Wanachama wa NSSF. Mradi wa Dungu Farm satelite town unatarajiwa kuanza katika mwaka huu wa fedha....