Frequently Asked Questions
Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport size. Baada ya kuandikishwa utapatiwa kitambulisho cha uanachama kitakachokuwezesha kuanza kuchangia katika akaunti yako ya uanachama.
Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi.
Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa na NSSF. Tafadhali fika ofisi za NSSF kwa maelekezo zaidi.