Mafao haya hulipwa kwa wanachama wanawake wanaotegemea kujifungua au wameshajifungua.
Sifa Zinazotakiwa.
- Awe amechangia angalau michango 36 kati ya hiyo michango 12 iwe imefanywa karibu na wiki ya kujifungua
- Awe anategemea kujifungua au ameshajifungua mtoto
- Hulipwa kila baada ya miaka mitatu isipokuwa ikiwa mtoto atafariki ndani ya miezi 12 baada ya kuzaliwa.
- Madai yafanyike kabla ya kujifungua au ndani ya siku 90 baada ya kujifungua
Mafao yanayotolewa
- Mafao ya fedha taslimu
Mafao haya ni asilimia 100% ya wastani wa mapato ya siku ya mwanachama kwa kipindi cha miezi sita kabla ya wiki ya 20 ya ujauzito. Mafao haya hulipwa kwa muda wa wiki 12, sawa na mishahara ya miezi 3.
Malipo hufanyika kwa awamu mbili yaani wiki 4 kabla ya kujifungua na wiki 8 baada ya kujifungua. Mwananchama anaweza kuamua kulipwa kwa wiki zote 12 baada ya kujifungua.
- Mafao ya Matibabu
Matibabu hutolewa kwa magonjwa yanayoambatana na ujauzito wa mwanachama. Matibabu huanza kutolewa baada ya wiki ya 24 ya ujauzito na huishia masaa 48 baada ya kujifungua au siku 7 ikiwa kajifungua kwa upasuaji. Matibabu haya hufanywa na hospitali ambazo zimeingia mkataba na Shirika wa kutibu wanachama wa NSSF