Pensheni hii hulipwa kwa mwanachama aliyepoteza angalau theuthi mbili (2/3) ya uwezo wake wa kufanya kazi kutokana na ulemavu wa kimwili au kiakili kama utakavyothibitishwa na Bodi ya Madaktari.
Sifa Zinazotakiwa.
- Uthibitisho wa Bodi ya Madaktari wa kupoteza 2/3 ya uwezo wa kufanya kazi.
- Michango 180 au angalau 36 kati yake michago 12 iwe imelipwa karibu na kupata ulemavu
- Awe chini ya umri wa kustaafu
Mafao Yanayotolewa
- Ukokotoaji wa pensheni ya ulemavu ni sawa na ule wa pensheni ya uzee isipokuwa huongezwa 1% kwa kila michango 12 inayozidi kiwango cha michango 180
- Mafao yanayotolewa ni sawa pia na mafao ya pensheni ya uzee yaani pensheni ya kila mwezi, mkupuo wa awali na mkupuo maalum kwa aliyekosa sifa zinazotakiwa.
- Pensheni hulipwa hadi mwanachama atakapofariki au atakapotimiza umri wa kustaafu na kuhamia pensheni ya uzee.