News Archive

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) inashiriki katika maonyesho ya Nanenae yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. Kauli mbiu ya maonyesho ya Nanenane mwaka 2018 ni ‘’Wekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda’’

Katika maonyesho ya Nanenane Mkoani Simiyu NSSF inatoa huduma mbalimbali zikiwemo elimu kwa umma juu ya Wakulima Scheme. Lengo la Wakulima Scheme ni kutoa mafao yote yanayotolewa na NSSF kwa wanachama walio katika sekta ya kilimo. Kwa kujiunga na NSSF wakulima na familia zao wanaweza pata matibabu ya bure, pia NSSF inawawezesha kupata mikopo ya riba nafuu kwaajili ya kununulia pembejeo, kusomesha watoto wao na kufanya shughuli zingine za kimaendelo.

Huduma zingine zinazotolewa katika banda la NSSF ni pamoja na elimu ya mafao na umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa watu walio katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kuadikisha wanachama wapya, kutoa taarifa za michango ya wanachama na maelezo juu ya miradi ya nyumba zinazouzwa na Shirika, viwanja na majengo ya kupangisha.

NSSF inawakaribisha wakazi wote wa Simiyu na maeneo ya jirani wafike katika banda la NSSF lililopo pembeni ya mabanda ya Benki ya NMB na NBC ili waweze kupata huduma za NSSF kwaajili ya kuboresha maisha ya sasa na baadae.

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Omary Mgumba akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Kilimo Prof. Siza Tumbo katika banda la NSSF Nanenane Simiyu

Afisa wa NSSF Hamisi Duma akitoa maelezo kwa wakina mama waliotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu

Maafisa wa NSSF Mario Zemba na Mselem Mwanamsoga wakitoa maelezo kwa mwanachama aliyetembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu

 

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4