News Archive

Wanananchi mbali mbali wanaendelea kujitokeza kwa wingi kujiunga na mfumo wa Hiari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kupitia  kampeni ya Zamu Yako. Mfumo wa Hiari utawawezesha kujiwekea akiba ya maisha yao ya baadae pindi wanapofikia umri wa kustaafu.

 

Kampeni hii ya sasa ya Zamu Yako ni maalumu kwa Watanzania wote ambao wako kwenye sekta isiyorasmi wa hapa nchini ambao wamejiajiri wenyewe katika shughuli mbali mbali za kujiongezea kipato.

Afisa mwandamizi wa matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ABBAS COTHEMA amesema kuwa wananchi wengi wanaendelea kujitokeza kwa wingi baada ya kuelewa kuhusiana na mifuko ya hifadhi ya jamii jambo ambalo linaonyesha mafanikio makubwa sana katika kampeni hii.

“Kwa kweli uelewa kwa sasa kwa wananchi ni  wa hali ya juu kwani wengi huamua kujiandikisha na mpango huu wa Hiari bila kushurutishwa na mtu yeyote, haya ni mafanikio makubwa sana kwa NSSF” alisema Cothema .

Cothema amesema kuwa kwa sasa wanaendelea na kampeni hii katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Dar es Salaam baada ya kupata maombi mengi kwa wadau wanaofanya shughuli mbali mbali za kijamii na hivyo wanahamasisha na kuandikisha wananchi kujiunga na NSSF.

Kwa mujibu wa Cothema mpaka sasa wameshawafikia wananchi wengi zaidi katika mikoa 15 ambao wamejiunga na mpango huo wa Hiari.

Pia Cothema amesema kwamba wanashukuru kwa sasa wananchi wanaendelea kuelewa kuhusiana na umuhimu wa kujiandikisha kwa hiari jambo ambalo linapelekea baadhi ya vikundi vinavyojumuisha wajasiriamali kuendelea kutoa maombi ya wananchama wao kupewa elimu ya kujiwekea akiba na baadae waweze kujiunga kwenye mpango huo wa Hiari.

Kiwango cha chini cha kuchangia kwenye mpango huo wa Hiari ni kuanzia kiasi cha shilingi elfu ishirini na kuendelea ambapo mwanachama  anayejiunga anafaidika na mafao sita yanayotolewa na NSSF yakiwemo mafao ya pesheni ya uzeeni  na matibabu bure kwa mwanachama, mwenza wake na watoto wake wanne(watoto) wasiozidi umri wa  miaka 18 au 21 kama bado wanasoma.

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4