emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

MKURUGENZI MKUU WA NSSF ATAJA VIPAUMBELE SABA MUHIMU ‘KUFYEKA’ KERO ZA WANACHAMA





Na MWANDISHI WETU



Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amemuhakikishia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, kuwa katika mpango na bajeti ya Mfuko ya mwaka ujao wa fedha yaani 2021/2022, wamejikita zaidi katika vipaumbele saba ambavyo vinaenda kuondoa kero mbalimbali hasa za wanachama.



Mshomba alisema hayo mwishoni mwa wiki, wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la 47 la Wafanyakazi wa NSSF lililofanyika Mkoani Morogoro.



1.KUANDIKISHA WANACHAMA SEKTA BINAFSI NA SEKTA ISIYO RASMI
Alitaja kipaumbele cha kwanza, ni kuhakikisha wanaandikisha wanachama katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi



2.KUBORESHA HUDUMA KWA WANACHAMA
Kipaumbele cha pili, Mshomba alisema ni uboreshaji wa huduma kwani kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wanachama, hivyo wameelekeza nguvu katika kulitekeleza hilo.



“Tutahakikisha mifumo yetu (NSSF), iko vizuri na inakidhi matarajio yetu, katika hili tutatumia Tehama kuhahikikisha kazi zetu zinakwenda vizuri na huduma kwa wateja zinatolewa,” alisema.



3.MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI
Mshomba alisema kipaumbele cha tatu, ni mafunzo kwa wafanyakazi ili waweze kuelewa taratibu za Mfuko.



4 MAFUNZO YA WATOA HUDUMA KWA WANACHAMA
Kipaumbele cha nne ni mafunzo kwa Wafanyakazi watoa huduma kwa wanachama ili waweze kuvaa viatu vya WANACHAMA kwa kuzingatia maadili ya Mfuko.



5.KUJENGA TIMU MOJA MIONGONI MWA WAFANYAKAZI
Alisema kipaumbele cha tano, ni kujenga timu mmoja kwani bila ya kuwa na timu moja katika Mfuko mkubwa kama huo wanaweza wasifikie malengo, hivyo watawafanya wafanyakazi kuwa sehemu ya Mfuko huo.



6.KUWEKA MAZINGIRA BORA YA KAZI
Mkurugenzi Mkuu huyo alisema kipaumbele cha sita, wataweka mazingira bora ya kazi kwani ni jambo muhimu na kwamba amemuomba Waziri Jenista kuwaunga mkono.



7. USIMAMIZI MADHUBUTI WA MENEJIMENTI NA BODI
Kipaumbele cha saba, alisema ni usimamizi madhubuti hasa kwa Menejimenti na Bodi kwamba katika kutoa huduma bora lazima usimamizi uwe madhubuti ili waweze kufanikiwa katika malengo yao.