emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​​WANAFUNZI ELIMU YA JUU WAZIDI KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII- NSSF



Meneja wa Sekta Isiyo Rasmi wa NSSF,Rehema Chuma akitoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii na uwekaji wa akiba katika Mfuko kupitia Mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi. Semina kuhusu hifadhi ya jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ilifanyika mwishoni mwa wiki.

WANAFUNZI ELIMU YA JUU WAZIDI KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII- NSSF

Meneja wa Sekta Isiyo Rasmi wa NSSF,Rehema Chuma (Hayupo Pichani) akitoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii na uwekaji wa akiba katika Mfuko kupitia Mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi. Semina kuhusu hifadhi ya jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ilifanyika mwishoni mwa wiki.

NSSF NA WANACHUO

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma namna wanavyoweza kuchangamkia fursa ya kujiwekea akiba kupitia NSSF.

Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao pia ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakihamasisha Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma kujiunga na kuchangia NSSF ikiwa ni moja ya fursa muhimu ya kutimiza malengo yao pindi watakapokuwa wamemaliza masomo yao.

FAIDA YA KUWA MWANACHAMA WA NSSF

Bi. Lulu Mengele, Meneja Uhususiano na Elimu kwa Umma NSSF akieleza faida ya kuwa mwanachama wa NSSF wakati alipokuwa anatoa elimu kwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Elimu kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu ni moja ya mkakati wa kuhakikisha kuwa jamii inatambua umuhimu na faida ya hifadhi ya jamii kwa wote sekta rasmi na sekta isiyo rasmi.

ELIMU

Afisa Mkuu sekta isiyo rasmi wa NSSF,Macdonald Maganga akitoa elimu ya jinsi ya kuwasilisha michango NSSF kwa wanachuo wa chuo kikuu cha Dodoma kupitia mpango wa Taifa wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi.