emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

NSSF Schemes

Wakulima Scheme


Malengo

 • Kutoa mafao yote yatolewayo na NSSF kwa wanachama wa sekta ya Kilimo.
 • Kuwapa wakulima na familia zao matibabu ya bure ili wawe na afya bora ya kuweza kendesha kilimo bora
 • Kusaidiana na serikali kupunguza umaskini kwa jamii.
 • Kuwawezesha wakulima kupata mikopo ya riba nafuu sana kwa ajili ya kununulia pembejeo,kusomesha watoto wao,na shughuli nyingine za maendeleo.
 • Kunusuru kipato ambacho wangekitumia katika matibabu na badala yake wakitumie kujiendeleza kiuchumi na kuweza kurejesha mikopo popote walipokopa.
 • Kuwawezesha wakulima kupata mafao ya pensheni wakati watakapokuwa wazee na kushindwa kuendelea na kilimo.

Wanaohusika na Mpango huu

 • Wakulima wote waliojiunga na vyama vya msingi vya mazao (AMCOS) au vyama vingine vyovyote vya ushirika.
 • Mkulima mmojammoja ilimradi awe na uhakika wa kuweza kuchangia japo Tshs. 20,000/- na kuendelea kwa kila mwezi
 • Watu wote wanaojishghulisha na biashara zote za kilimo ikiwemo ununuzi wa mazao, usafirishaji, usindikaji, uongezaji thamani (Agri prossessing), uuzaji wa mazao na yale yote yatokanayo na mazao ya kilimo.
 • Watu wote wanaojishughulisha na ufugaji wa wanyama,nyuki, uwindaji,na uvuvi,pamoja na wale wote wanaojisghulisha na biashara ya mazao yatokanayo na shughuli zilizotajwa hapo juu.
 • Wanachama walio katika mifuko mingine ila wakapenda kujiunga kwa mfumo wa hiari ili kupata mafao yatolewayo na NSSF. Wanachama wanaopata
 • pensheni ya NSSF na wakawa radhi kukatwa asilimia sita(6%) ya pensheni yao ili kuweza kupata huduma ya matibabu.