Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi Christopher Chiza ametembelea miradi ya NSSF Kigamboni. Katika Ziara hiyo miradi aliyotembelea ni pamoja na Daraja la Kigamboni, Mradi wa Nyumba za Makazi Mtoni kijichi na Mradi wa Nyumba wa Dege Eco Village.


Waziri  Christopher Chiza ameisifia NSSF kwa juhudi zake za ujenzi wa nyumba ambazo zitawasaidia Watanzania na Wageni kupata makazi bora.
Pia amesema "Nimefurahishwa saana na  ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambao unaendelea  kukamilika kwa Daraja la Kigamboni kutafungua fursa za uwekezaji katika mji wa Kigamboni ambao unakuwa kwa kasi sana".