Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), linaendesha kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Tanga.
Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.


Zoezi hili litakaloanzia mkoani Tanga. Linatarajiwa kwenda Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Zoezi hili linafanyika katika viwanja vya Tangamano kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.

 
HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA


Huduma mbalimbali zitatolewa bure kwenye kambi hizi zikiwemo;
• Upimaji wa Shinikizo la damu
• Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
• Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Uzito)
• Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo
• Ushauri nasaha na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
• Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.


Huduma zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.


NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa Tanga kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Wavuvi, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.


Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS, pamoja na Mafao bora mengineyo.
Wananchi wa Tanga wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure

Benefits Menu

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1