emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

BARABARA YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 99


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ndg. William Erio, amekagua ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wa kipande cha barabara kinachounganisha Daraja la Nyerere, na Kigamboni. Kulingana na maelezi ya kitaalamu ya Mhandisi Mkazi Simon Mgani, ujenzi huo umekamilika kwa zaidi ya asilimia 99. Mhandisi Mgani ambaye ni msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS alisema kwa sasa hawawezi kuikabidhi rasmi barabara hiyo kwa sababu wanaiweka katika hali ya usalama, kwani barabara ni pana, hivyo inahitaji kugawanywa kwa rangi nyeupe na njano ili kutenganisha magari yanayokwenda sehemu tofauti tofauti.


Mhandisi Mgani alisema kitaalamu rangi inatakiwa ipakwe baada ya lami kukauka vizuri ili iweze kushika vizuri, kazi ambayo itachukua muda wa wiki mbili.


Katika ziara hiyo Erio aliambatana na baadhi ya wafanyakazi wa NSSF.