emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

NSSF Schemes

INFORMAL SECTOR

MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII

MFUMO WA HIFADI YA JAMII WA KITAIFA KWA SEKTA ISIYO RASMI


1.Mfumo wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta isiyo rasmiShirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) hutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa wanachama walioajiriwa kwenye Sekta Binafsi na waliojiajiri wenyewe kwenye Sekta isiyo Rasmi chini ya kifungu cha 6 cha sheria ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii sura ya 58 marejeo ya mwaka 2018. Ili kuwahudumia vizuri na kwa ueledi wanachama waliojiajiri wenyewe kwenye Sekta isiyo rasmi Shirika limeanzisha Mfumo wa Kitaifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta isiyo Rasmi (National Informal Sector Scheme – NISS).Sababu za kuanzisha Mfumo wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta isiyo rasmi;

Kuongeza wigo wa wanachama kwa kutoa fursa ya Hifadhi ya Jamii kwa makundi ambayo hayanufaiki na huduma hizi ingawa wanashiriki kikamilifu kuchangia Uchumi wa Nchi.

Kusaidia Juhudi za Serikali za kupunguza umaskini wa kipato kwa wananchi,

Kushiriki kuongeza nguvu za uzalishaji mali na kukuza uchumi wa Nchi,

Kuchochea kasi ya maendeleo ya uchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

2.Wanaonufaika na utaratibu huu

Watu wote waliojiajiri wenyewe kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wa madini, wafanyabiashara ndogo ndogo n.k

Walioko kwenye ajira na ambao wanapendelea kujiwekea akiba ya ziada chini ya Mfumo huu.

3.Namna ya kujiandikisha kuwa mwanachama

Mwanachama atasajiliwa kwenye Mfumo huu wa Hifadhi ya jamii wa sekta isiyo rasmi akiwa na vielelezo vifuatavyo;

Awe na namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA)

Awe na picha moja

Baadhi ya wanachama watatakiwa kutoa mchango wa awali usiopungua shilingi ishirini elfu (20,000/=) kama mchango wa mwezi.

4.Taratibu za kujiandikisha

Mwanachama atajaza fomu ambayo imeambatanishwa na namba ya kitambulisho cha taifa pamoja na picha moja ( passportsize)

Baadhi ya wanachama watatakiwa kuwasilisha risiti ya malipo ya mchango wa awali.

5.MichangoMwanachama atachangia kiwango kisichopungua shilingi elfu ishirini (20,000/=) kwa mwezi au zaidi.

6.MafaoMafao yanayopatikana katika Mfumo wa Kitaifa wa sekta isiyo rasmi ni;

Mafao ya uzeeni ( Old Age Pension)

Mafao ya matibabu chini ya utaratibu maalumu

Mafao ya mikopo

Mikopo inayotolewa sasa ni ya Uanzishwaji wa viwanda ambapo mtu mmoja mmoja au kikundi wanaweza kukopeshwa kuanzia shilingi milioni nane (8,000,000.00) hadi shilingi milioni mia tano (500,000,000.00)

NSSF MAKAO MAKUU

Jengo la Benjamin Mkapa Pension Towers

S.L.P 1322, Dar Es Salaam

Simu:+255 22 2163400-19 au +255 75 6140140

Nukushi: +255 22 2200037

Barua pepe: dg@nssf.or.tz